JOYCE KIRIA AONYESHWA ALIPO MUMEWE
0
Bw.Henry Kileo akiwa na watuhumiwa
wenzake wa mashtaka ya Ugaidi yanayowakabili wakati walipofikishwa
Mahakama ya Hakimu mkazi mkoani Tabora kwa mara ya kwanza
Wanachama wengine wa Chadema ambao
wanahusishwa katika mashataka hayo ya Kigaidi ambapo imedaiwa kuwa
watuhumiwa walifanya makosa hayo ya Ugaidi na kumjeruhi Bw.Mussa Tesha
ambaye ni mwanachama wa CCM wakati wa kampeni za uchaguzi wa Ubunge wa
jimbo la Igunga mnamo tarehe 9/9/2011 katika msitu wa Hanihani huko
wilayani Igunga.
Ulinzi katika Mahakama hiyo uliimarishwa ipasavyo.
Kamanda Henry Kileo akiwa ndani ya
gari pamoja na watuhumiwa wenzake wanne wakisubiri kupelekwa Gereza la
Mahabusu hadi watakapoletwa tena Mahakamani hapo mnamo tarehe 8/7/2013
Na Josephat Isango wa Tanzania Daima
KAIMU Katibu wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA), Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kilewo,
anashikiliwa na polisi , akihusishwa na tukio la kumwagiwa tindikali,
Musa Tesha. Tesha alimwagiwa tindikali na watu wasiojulikana Septemba 9,
mwaka juzi kwenye kampeni ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga,
uliomuweka madarakani Dk. Kafumu Dalali.
Akizungumza juzi na Tanzania Daima
kabla ya kufika makao makuu ya Jeshi la Polisi, Kilewo alisema hajui
anachoitiwa na kwamba anatekeleza wito wa jeshi hilo kuwa afike ofisini
kwao. “Sijui ninachoitiwa, nimepigiwa simu naenda kutekeleza wito,
nimesha wataarifu mawakili wangu ninaowaamini, kwa kuwa chochote
kinaweza kutokea cha msingi Watanzania wapenda mageuzi waniombee kwa
Mungu,” alisema Kilewo.
Wakili wa Kilewo, Peter Kibatala,
alisema baada ya mteja wake kuhojiwa kwa muda wa saa tano juzi alielezwa
kuwa anapelekwa Igunga, mkoani Tabora kuunganishwa na watuhumiwa
wengine katika kesi ya kutumia tindikali na kujeruhi.
Kibatala alisema anasikitishwa na
hatua ya jeshi hilo kumnyima dhamana mteja wake ilhali kosa
wanalomtuhumu linadhaminika na kwamba hayo ni matumizi mabaya ya
madaraka kumzuia mtu kwa zaidi ya saa 24 pasipo kumfikisha mahakamani.
Wengine wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kutumia
tindikali na kudhuru watu ni pamoja na Oscar Kaijage wa Shinyanga na
Evodius Justinian wa Bukoba.
Evodius Justinian alikamatwa na
Jeshi la Polisi mjini Bukoba na kushikiliwa kwa siku kadhaa kabla ya
kusafirishwa hadi jijini Dar es Salaam. Kabla ya kusafirishwa na
kufikishwa jijini Da r es Salaam, Justinian alieleza kuteswa na kupigwa
na askari waliokuwa wakimzuia katika vituo mbalimbali kuanzia mjini
Bukoba.