PRODUCER LUCCI AAMUA KUMVISHA PETE MCHUMBA WAKE BAADA YA KUTUHUMIWA ANATOKA NA JOKATE

0
Hivi sasa producer wa wimbo wa" kaka dada" ameamua kumvisha pete mpenzi wake ambaye amekuwa mchumba wake rasmi.

Akiongea na millardayo,Lucci alikuwa na haya ya kusema:

“Baada ya mambo ya project ya Kaka Dada kukamilika nimeona ni muda muafaka kabisa kumvisha pete mpenzi wangu Lisa Semgeliwa au marafiki zake huwa wanamuita Lizzyblazzer.

"Unajua like seriously tumekuwa kwenye dating kwa muda zaidi ya miaka 2. Muda huo unatosha kabisa naamini ni vizuri kuingia kwenye hatua nyingine ya mahusiano yetu” .



Wengi wanajiuliza, huyu shemeji yetu alikuwa na hali gani kipindi kifupi kilichopita wakati "Kaka Dada" ikiwa JIKONI na baada ya kutoka????...

Lucci analitolea ufafanuzi jambo hilo:
”Unajua ukishakuwa kwenye mapenzi na mtu anayejitambua na anaefahamu kazi yako. Basi atafahamu kabisa entertainment inahitaji vitu tofauti ili kufanikisha.

"So mimi na yeye tuliongea kwamba muda huu tunaitoa kazi ya kaka dada na plan nzima alikuwa anaijua. So hakukuwa na tatizo lolote”

Baada ya maelezo hayo,Lucci aliamua kuelezea kuhusu mchumba wake:

”Lisa ni director wa kampuni yetu mimi na yeye inaitwa Tsere. Kazi tunayofanya ni creative and marketing, pia anafanya kazi ya HR kwenye hii kampuni”

Ni imani yangu kuwa Lucci ameamua kufunguka ili kuzima tuhuma zilizokuwa zikisambaa kwa kasi kuhusu kutoka kimapenzi na Jokate.

0 comments: