RAY C AFUNGUKA KUHUSU MAISHA YAKE MAPYA BAADA YA KIMYA KIREFU

0

 

Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu, hitmaker wa Niwe Nawe Milele, Rehema Chalamila aka Ray C anatarajia kurejea tena kwa kishindo kwenye muziki. Ray C anatarajia kuonekana rasmi kwenye shughuli za kawaida na za muziki wiki ijayo. Soma habari zake hapa chini;


Kuhusu kama yupo tayari kufanya muziki

I am more than ready, wakati nipo huku nilikuwa naandika andika nina nyimbo kama tatu nne hivi kali sana. Sema ningependa tu kuwaambia mashabiki wawe na uvumilivu kwasababu wameniombea sana na wengi kwenye Instagram, Facebook walikuwa ‘when are you coming back, we miss you’ vitu kama hivyo. Na mimi ningependa kuwaambia tu kwamba wiki ijayo ndio narudi rasmi, kwa wale ambao walikuwa na wasiwasi, ‘where is Ray C, Ray C atarudi tena kwenye muziki’ na vitu kama hivyo. Tutaanza kuingia studio next week, kila kitu kitaanza next week. Lakini kama nyimbo kuandika na kila kitu vyote viko tayari.
Kuhusu aina ya nyimbo atakazokuwa akiimba zaidi
Nafikiri sasa hivi ntabase kwenye maisha zaidi. Nafikiri watu wanahitaji kujua mambo ya maisha zaidi. Unajua mimi tangu mwanzo nilikuwa naimba mapenzi, ofcourse nyimbo za mapenzi zitakuwepo sema ntabase zaidi kwenye mambo ya maisha.
Kuhusu mabadiliko aliyonayo sasa
Ray C ni kibonge sasa hivi, Ray C amenenepa kidogo. Najua mashabiki wakiangalia kwenye Instagram wanasema ‘dada vipi bana’ lakini najua njiani huko ntapunguapungua. Lakini Ray C wa sasa hivi sio kale kembambaa kale mlikokazoea kale. Sasa hivi Ray C kidogo amevuta shavu kwahiyo wakiniona wasishangae. Halafu pia kwa sauti niko fit sana. Yaani all along nilikuwa nafanya zaidi mazoezi kwasababu nimepata sana muda wa kupumzika, mazoezi ya kuimba, yaani nimeona nipo tofauti na zamani.
Kuhusu sababu za kunenepa
Si unajua tena maisha mazuri, kula kula vizuri, kutulia kwa muda bila kufanya kazi ndio maana nikafutuka kidogo lakini ntafanya mazoezi, ntapungua si unajua lazima nipungue kidogo ili niweze kuimiliki stage,vile nilivyokuwa zamani au better zaidi.
Kuhusu wasanii wapya anaowasikiliza
Namsikiliza sana ambaye namkubali ni mdogo wangu Recho. I think kwasababu muziki wake kidogo umefanana na wangu kwahiyo napenda ladha yake halafu kuna Diamond pia namsikiliza, ni msanii ambaye anafanya vizuri sasa hivi kwahiyo namsikiliza pia kuna kitu gani hapo watu wanakipendea zaidi niibeibe maideas hapo nifanye kazi nzuri.

Kuhusu alivyojiskia baada ya kusikia nyimbo za Recho

Recho mimi namjua kabla hajatoka na alikuwa anapenda sana nyimbo zangu, alikuwa anasikiliza sana nyimbo zangu. Mara ya kwanza nimemuona alikuja akaniambia ‘dada Rehema naomba nikuimbie wimbo mmoja’ akaniimbia ‘Umenikataa Bila Sababu’, akaniimbia nyimbo kama tatu hivi. Kwahiyo namjua kabla hata hajaingia studio. Kwahiyo nilikuwa najua kabisa nimemuinfluence kiasi gani.

0 comments: