SUGU AACHIWA HURU KWA DHAMANA
0
MBUNGE wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (SUGU) amekamatwa na Jeshi la Polisi Mjini Dodoma na kuachiwa kwa dhamana.
Mwandishi wetu akiwa Mjini Dodoma anasema kwamba Mbunge huyo alikamatwa muda mfupi baada ya kutoka katika vikao vya Bunge.
Sugu alikamatwa na kupelekwa katika
Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma na baada ya kuhojiwa aliachiwa kwa dhamana
na kutakiwa kuripoti kituoni hapo kesho asubuhi kwa mahojiano mengine.