DIAMOND NA WEMA WARUDIANA

0

 



Baada ya habari kuenea kuwa Diamond PLatnumz amerudiana na Wema walipokuwa Malaysia katika moja ya show zake na Platnumz kukanusha habari hiyo kupitia website yake, hatimaye BK imepata picha nyingi za Diamond na C.E.O wa Endless Fame Wema Sepetu wakiwa kwenye pozi tofauti tofauti za kimahaba nchini humo.



           

Baadhi ya picha hizo, moja inawaonesha Diamond na Wema wakiwa wamevaa Mapajama (nguo za kulalia) sehemu kama hotelini hivi na nyingine ikimuonesha Diamond akim-kiss Wema wakiwa kitaa. Lakini Diamond ni real boyfriend wa Penny…

Kupitia account yake ya instagram diamondplatnumz amepost moja ya picha zilizopo katika movie mpya aliyoshirikiana na mwanadada wema sepetu kuonyesha msisitizo ktk hilo diamond amesema haya:

 
diamondplatnumz
: Katika moja ya Muvie ambazo naimani itakuwa ni Gumzo, Mfano na Bora toka Tanzania basi ni hii... #TEMPTATIONS .... STAY TUNED!!!! SOON!....#DayOne #Location #SomeWhere   


USHAISOMA HII? WEMA, DIAMOND WARUDIANA

0
WACHUMBA wa zamani, Wema Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond’ ndiyo habari ya mjini kwa sasa, kwamba wawili hao wamerudiana tena kwa kasi kupita ile ya mwanzo, Amani limechimbua.
Habari zinasema wawili hao walikutana Dubai hivi karibuni  kabla Diamond hajaenda Malaysia na Wema akiwa njiani kuelekea Hong Kong, China ambapo walikula bata kwa sana.
Ikazidi kuelezwa kuwa wameamua kuwa kwenye uhusiano wa siri na lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha mpenzi wa sasa wa msanii huyo wa Bongo Fleva, Penniel Mungilwa ‘Penny’ hajui kitu chochote.

TAARIFA ILIVYO
Kwa muda wa siku nne, ndani ya mitandao ya kijamii hasa kwenye Instagram, maneno yenye kuashiria kuwa wawili hao wapo pamoja tena yamekuwa yakichukua nafasi.
Baada ya kusambaa kwa habari hizo, Penny naye alitupia picha yake akiwa kitandani na Diamond na kuandika kuwa waachwe kama walivyo.
Ndani ya mtandao wa Instagram yakazuka makundi mawili, upande wa mawifi wa Penny, akiwemo Halima Kimwana na kundi lingine la mawifi wa upande wa Wema.
Kundi la Wema waliandika kuwa mwanamke anayependwa na ndugu wa mume siku zote mwanamme huwa hampendi hivyo Wema ni mpenzi sahihi wa Diamond kwa vile hapendwi na ndugu kama Penny.

MBAYA ZAIDI
Mbaya zaidi, katika hali isiyotegemewa kwenye akaunti yake ya Instagram, Wema alitupia wimbo mpya wa Diamond uitwao My Number One na kuweka maoni yake kwamba anaupenda wimbo huo.
Wengine waliochangia walisema Wema ana lake jambo kwa Penny kwa vile si jambo jepesi kusifia wimbo wa mwanamme ambaye alikuwa mpenzi wake na sasa ana mwingine anayejulikana, yaani Penny.

PICHA YA WEMA SASA
Wema hakuishia kuposti wimbo huo tu, alikwenda mbele zaidi kwa kutupia picha yake yenye pozi tamu na kuuliza; huyu hapa baby wa nani huyu? (yaani yeye).
Wengi walimsifia lakini wengine walifunguka kwa kusema ni baby wa Diamond, jambo ambalo Wema hakulipinga.

PENNY AONGEA NA AMANI
Kufuatia kuenea kwa habari hizo, Amani lilianza kuwasaka watu watatu ambao ndiyo wenye uwezo wa kubainisha ukweli au uongo wa ishu hiyo iliyoenea mjini.
Watu hao ni Diamond mwenyewe, Wema anayedaiwa kurudiwa na Penny, mpenzi wa sasa wa Diamond.
Wa kwanza kupatikana alikuwa Penny ambapo alipoulizwa kuhusu kuwepo kwa madai hayo alifunguka:

AKIRI KUNYETISHIWA
“Ni kweli hata mimi nimenyetishiwa habari hizo lakini siamini kama inawezekana hao watu wakarudiana.

ASEMA KUNA KUNDI LINAPANGA NJAMA
“Nijuavyo mimi kuna kundi la watu ambao wapo upande wa pili (wa Wema) ndiyo wanaoeneza hizo habari, pengine wanataka niamini kisha nimwache Diamond, simuachi ng’o.

ANATAKA USHAHIDI
WA PICHA
“Kama niliweza kumvumilia kwa kuona picha akiwa na Irene Uwoya hotelini sembuse hili la safari hii hata picha hakuna?”

ALISHAMUULIZA DIAMOND
“Mimi nilishamuuliza Diamond, japo hakusema ni kweli au uongo ila aliniambia achana na hizo habari.”

DIAMOND APIGA KIMYA
Baada ya kuongea na Penny,
 lilimpigia simu Diamond ambapo alipokea na kusema yuko kikaoni na kumtaka paparazi kupiga baadaye. Hiyo ilikuwa saa 4:16 asubuhi ya juzi.
Saa 7:11 mchana, Diamond alipigiwa simu tena lakini hakupokea. Akatumiwa meseji ya kumkumbushia, hakujibu. Akatumiwa meseji yenye madai ambayo pia hakuijibu.

MAMA WEMA KABLA YA KUULIZWA AFUNGUKIA MADAWA YA KULEVYA
Amani liligundua Wema bado yupo Hong Kong hivyo liliamua kumpigia simu mama yake, Bi. Miriam Sepetu ili kuomba namba ya bintiye, lakini kabla ya ombi hali ikawa hivi:
“We nani, hivi kuna gazeti moja limeandika eti mwanangu amekamatwa na madawa ya kulevya China anasubiri kunyongwa, ni akina nani wale, wana akili kweli?
“Mimi sikubali safari hii, tutafikishana kwa mwanasheria wangu.
“Tena ukikutana nao waambie waache kumzushia mwanangu, wasimtie mkosi bure, hajakamatwa yupo salama kabisa.”
Mpaka sasa ushahidi wa kuonesha wapenzi hao wa zamani kuwa  wamerudiana bado haujawekwa hadharani.
Source:GPL

MKE WA WAZIRI WA ZANZIBAR ATAPELIWA NA VIJANA WALIOJIFANYA WAGANGA NA WALIOTAKA KUMTAJIRI KWA NJIA YA MIZIMU...STORI KAMILI ILIKUAJE NI HAPA

0


Wapigaji wanazidi kuiteka nchi, uthubutu wa vitendo vya uporaji kwa njia za udanganyifu umeshika kasi na sasa hivi umepiga hodi kwa mke wa waziri wa zamani.
Ikupa Mwakanjuki, mke wa waziri wa zamani wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, marehemu Brigedia Adam Mwakanjuki, ametapeliwa shilingi milioni 280.
Waliomtapeli Ikupa ni vijana wanne ambao inadaiwa ni matapeli wazoefu jijini Dar es Salaam na kwenye baadhi ya mikoa ya Tanzania, wakitumia ‘triki’ ya uganga wa kienyeji.
Vijana hao wakijifanya waganga wa kienyeji, walimfuata Ikupa na kumwambia kwamba wangeweza kumfanya atajirike zaidi kwa njia za mizimu.
Watuhumiwa wote wanne wa utapeli huo wameshakamatwa lakini tumepata majina ya wawili, wa kwanza akifahamika zaidi kwa jina la Silver na mwingine ni Mwang’ombe ambaye picha yake inaonekana hapo chini.
Chanzo chetu kilisema kuwa baada ya mwanamke huyo kupewa maneno ya ulaghai, aliingilika lakini akawa hana fedha ambazo ‘waganga’ hao walizihitaji.
“Mama aliposema hana fedha, wale matapeli walimwambia anazo mali ambazo anaweza kuuza na kupata kiasi cha fedha kinachohitajika,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:
“Mama alisema analo shamba, wakamshawishi auze. Mama naye sijui aliwekewa nini, akawa anafanya kila kitu kutokana na maelekezo ya wale matapeli.

“Kweli aliuza shamba lakini fedha zote alikabidhi kwa wale matapeli. Siku zikapita, haoni mabadiliko yoyote, ghafla akamuona Mwang’ombe anaendesha gari la kifahari aina ya Toyota Land Cruiser Prado.
“Hapo ndiyo akashtuka, Mwang’ombe bila woga, akarudi tena kwa mama akamwambia zinahitajika fedha nyingine kwa ajili ya sadaka kwa yatima.
“Akiwa na wenzake, wakamshawishi auze shamba lingine zipatikane japo shilingi milioni 100 ili maisha yaanze kubadilika kwa kasi. Hapo ndipo akatushirikisha ndugu, tukagundua huo ni utapeli. Tukaamua kulifikisha hili suala kwenye vyombo vya sheria.”
Habari zaidi zinasema kuwa Ikupa kwa ushawishi wa ndugu zake, alifikisha malalamiko yake mpaka makao makuu ya jeshi la polisi na inadaiwa kuwa IGP Said Mwema aliagiza ma-RPC wote kufanya juu chini na kuwaweka nguvuni watuhumiwa.
“Hii ishu ni ya juu, sisi tumetumwa tuwakamate, tukishafanikiwa tutawakabidhi watuhumiwa kwa maofisa upelelezi makao makuu,” mmoja wa maofisa wa jeshi la polisi Kinondoni, alilinong’oneza .
Septemba 18, mwaka huu, saa 8 usiku, Mwang’ombe bila kujua kama yupo mtegoni, alipaki Prado lake lenye namba za usajili T940 CLX, Corner Bar, Sinza Afrika Sana, Dar es Salaam.
Alipopaki hapo, alichagua kiti ili apate ‘kuzila bata zake’ lakini eneo hilo, alikuwepo kaka mdogo wa Ikupa ambaye alitoa taarifa polisi na mara moja, gari lake likazingirwa kabla ya mtuhumiwa huyo kukamatwa na kufikishwa Kituo cha Polisi Kijitonyama, Mabatini.
Mwang’ombe alikamatwa Corner Bar na ndipo mtuhumiwa huyo alimtaja Silver kwamba naye ni mhusika.
Oparesheni ikitekelezwa na maofisa upelelezi makao makuu, ilifanikisha kukamatwa kwa Silver eneo la Kimara Baruti, usiku huohuo na siku iliyofuata, watuhumiwa wengine wawili walitiwa nguvuni kisha shauri likarejeshwa Oysterbay kwa utekelezaji wa mkondo wa kisheria.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Camillius Wambura, alilithibitishia  kwamba tukio hilo lipo mezani kwake.
“Tupo kwenye uchunguzi, kuna vitu tunakamilisha halafu baadaye tutafanya mawasiliano na ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa ajili kwenda mahakamani,” alisema Wambura.
Ikupa alipopigiwa simu, alipokea mtu wake wa karibu ambaye alisema: “Kama mama atataka kuzungumza na wewe atakupigia.”
Baada ya hapo hakupokea tena simu.
Utapeli kwa njia za uganga, mitandao ya simu, katika mashine za fedha (ATM) na kadhalika, umekuwa ukishika kasi nchini ingawa jeshi la polisi limekuwa likijipambanua kwamba linashughulikia kwa nguvu kubwa.

WANAOJIHUSISHA NA TINDIKALI KUKOMESHWA. HIKI NDICHO ALICHOKISEMA RAISI KIKWETE

0

RAIS Jakaya Kikwete amesema Serikali yake imedhamiria na itahakikisha inalimaliza tatizo la watu kumwagiwa tindikali, iwe ni Visiwani Zanzibar au Tanzania Bara. Katika kukabiliana na tatizo hilo, Rais Kikwete amesema hivi karibuni Jeshi la Polisi lilifanya operesheni katika mitaa ya Zanzibar na kukamata watu 10 wanaodaiwa kushiriki katika mipango ya kuandaa na kutekeleza matukio ya watu kumwagiwa tindikali.
Taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Dar es Salaam, ilisema Rais Kikwete alitoa kauli hiyo juzi jijini New York Marekani, alipokuwa akizungumza na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, baada ya kiongozi huyo wa Umoja wa Mataifa kutaka ufafanuzi wa suala hilo.
Kwa mujibu wa Rais Kikwete, chanzo cha tatizo la watu kumwagiwa tindikali lina sura nyingi, lakini kutokana na jinsi Serikali ilivyojipanga, tatizo litafikia mwisho baada ya siku chache.
“Ni kweli tumekuwa na vitendo hivyo, zaidi Visiwani Zanzibar kuliko Tanzania Bara ambako nako pia vimekuwapo vitendo hivyo.
“Ni jambo la kulaaniwa sana na hivi karibuni Jeshi la Polisi lilifanya operesheni maalumu na msako mkubwa Tanzania Visiwani ambako watu 10 walitiwa mbaroni na watafikishwa katika vyombo vya sheria baada ya taratibu za kisheria kukamilika.
“Wakati tatizo hili lilipoanza, tulidhani kuwa alikuwa ni Sheikh Soraga aliyekuwa anatafutwa peke yake na watu ambao walikuwa hawakubaliani kisiasa na msimamo wake, lakini mara wakaanza kushambuliwa watu wengine wakiwemo wasichana wawili wa Uingereza ambao walikuwa wanafanya kazi za kujitolea tu, lakini, tatizo hili ni lazima likome,” alisema Rais Kikwete.
Rais Kikwete ametoa msimamo huo wa Serikali wakati baadhi ya wananchi wameshadhurika kwa tindikali.
Miongoni mwao ni kiongozi maarufu wa Kiislamu Visiwani Zanzibar, Sheikh Soraga ambaye alimwagiwa tindikali wakati akifanya mazoezi ya viungo katika mitaa ya mji wa Unguja.
Mbali na huyo, viongozi wengine wa kidini wa Kanisa Katoliki visiwani humo, wameshamwagiwa kemikali hiyo na pia wasichana wawili raia wa Uingereza waliokuwa wakifanya kazi za kujitolea Visiwani Zanzibar, nao walimwagiwa kemikali hiyo.
Wasichana hao baada ya tukio hilo lililotokea mwezi uliopita, walisafirishwa kutoka Zanzibar na kuletwa Dar es Salaam kisha wakasafirishwa kwenda nyumbani kwao Uingereza kwa ajili ya matibabu zaidi.

MKUU WA WILAYA YA MBULU AWAPIGIA MAGOTI WANANCHI

0

Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, mkoani Manyara, Anatory Choya akiwa amewapigia wananchi magoti kwa maana ya kuonyesha unyenyekevu
 
Mbulu. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, mkoani Manyara, Anatory Choya, amesema kuwa aliwapigia magoti wananchi wa Kijiji cha Hydom, ili kuonyesha unyenyekevu kwa wananchi hao aliodai walionekana kujazwa maneno ya uchochezi na wanasiasa ili wavuruge amani .

Alisema kutokana fujo zilizofanywa na baadhi ya wananchi hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika majuzi, kwa nafasi yake angeweza kuagiza hata Jeshi la Polisi kuwadhibiti watu, lakini misingi ya dini yake haimruhusu kumdhuru mtu zaidi ya kumwonyesha unyenyekevu.
 
 

Alisema hali hiyo ndiyo iliyomfanya kuamua kupiga magoti na kumshtakia Mungu.

“Mimi ni mkristo, unyenyekevu ndiyo nguzo pekee ya kuonyesha upendo na kudumisha amani. Ningeweza kuagiza polisi wawadhibiti, lakini sioni sababu kwa kuwa hiyo siyo misingi ya utawala. Ndiyo maana nikaona bora nitumie njia nyingine ya kumshirikisha Mungu mbele yao,”alisema Choya na kuongeza:

“Wanasiasa wamekuwa wakipandikiza chuki kwa wananchi kwa makusudi kwa lengo la kuvuruga amani lakini kwa kumweka Mungu mbele nina imani tutafanikiwa ili siku moja tusije tukaingia kwenye mkumbo wa Syria na Misri”

Choya alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza na Mwananchi Jumapili, siku chache baada ya kitendo chake cha kupiga magoti mbeye ya wananchi kwenye mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Haydom.

Mkuu huyo wa wilaya alidaiwa pia kuwalaani baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Haydom kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kumdharau na kutofuata maagizo yake, wakati yeye amewasaidia katika kutatua migogoro mbalimbali waliyokuwa nayo.

Tukio hilo la kusikitisha lilijitokeza baada ya wananchi wa kijiji hicho kupinga agizo la Choya, lililowataka kufanya uchaguzi wa kaimu mwenyekiti wa kijiji hicho, kabla ya kufanya uchaguzi mdogo, ambapo walipinga kwa kudai kuwa hakuna sheria hiyo.

Mmoja wa wananchi hao alilumbana na mkuu huyo wa wilaya mbapo Choya alijibu; “Nami nitarudi kwetu." Naye Tikin akasema tena: “Unasema utarudi kwenu Biharamulo wakati hawakutaki kwani ulifukuzwa ubunge?”
Maneno hayo yalionyesha kumkwaza Choya ambapo alipiga magoti huku machozi yakimlenga na kumwomba Mungu afanye jambo kwa watu wa Haydom kwani wanamdharau kabla ya kujitokeza wazee watatu wa Haydom na kumwomba msamaha mkuu huyo wa wilaya