CHADEMA YAIBUKA KIDEDEA KATIKA UCHAGUZI HUKO ARUSHA

0

Uchaguzi uliofanyika jana Jumapili, Julai 14, 2013 wa kuwapata madiwani wa Kata Nne --Themi, Kaloleni, Kimandolu na Elerai-- za mkoani Arusha umemalizika. Huku Tume ya Uchaguzi ikisubiriwa kuwatangaza rasmi washindi, taarifa za awali zinasema kuwa CHADEMA imepata ushindi kwa kunyakua Kata zote Nne kama ifuatavyo:
 KATA YA THEMI: CHADEMA 678; CCM 326; CUF 313 
KATA YA KIMANDOLU: CHADEMA 2,665; CCM 1,169
 KATA YA KALOLENI: CHADEMA 1,019; CCM 389; CUF 169 
KATA YA ELERAI: CHADEMA 1,715; CCM 1,239; CUF 213 
Vyama vingine vilivyoshiriki vilikuwa ni TLP, CCK na Demokrasia Makini.

0 comments: