MFANYABIASHARA MWARABU MBARONI KWA KUMBAKA TAHIRA
0
JESHI
la polisi mkoani Ruvuma linamshikiria mfanyabiashara mmoja Jamali
Nassoro (67) mwenye asili ya kiarabu mkazi wa eneo la Making'inda katika
manispaa ya Songea kwa tuhuma za kumbaka na kumsababishia ujauzito wa
mimba ya miezi 5 msichana mwenye umri wa miaka 27 ambaye anadaiwa kuwa
na ugonjwa wa utindio wa ubongo(TAHIRA) ambaye jina lake tunalo
limehifadhiwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma
George Chiposi alisema kuwa tukio hilo la kukamatwa kwa mfanyabiashara
huyo mwenye asili ya kiarabu limetokea hivi karibuni baada ya wazazi wa
msichana kubaini kuwa mtoto wao yupo tofauti kimaumbile na kuchukuwa
jukumu la kwenda kumpima ambako vipimo vilionesha kuwa ni mjamzito wa
miezi 5.
Chiposi
alisema kuwa wazazi wa msichana huyo baada ya kubaini mtoto wao ni
mjamzito walimuhoji ili kujuwa ni nani aliyemfanyia unyama huo ambapo
licha ya kuwa msichana huyo ni tahira alieleza kwa shida kuwa alikamatwa
kwa nguvu na kulazimishwa kutoa nguo yake ya ndani na Nassoro ambaye
alimtaka ampelekee maji ya kuoga chumbani kwake.