Wahuni wavamia kanisa huko Rufiji waiba vifaa, ‘wajisaidia

0

Mkuu wa wilaya aahidi kuwasaka waliohusika hadi wapatikane na kufikishwa kwenye mikono ya sheria.

Rufiji. Watu wanaodhaniwa kuwa wezi Kijiji cha Mjawa, Kata ya Mjawa, wilayani hapa wamevunja mlango wa Kanisa Katoliki kijijini hapo kisha kujisaidia haja kubwa ndani ya kanisa  hilo, baadaye waliiba mali na samani mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Nurdin Babu, amelaani vikali tukio hilo na kuwataka waumini wa kanisa hilo kuwa watulivu wakati huu, huku akiahidi kuagiza polisi kufuatilia kwa karibu tukio hilo, ili wahusika wakamatwe na kufikishwa mahakamani.
Babu alisema watu waliofanya kitendo hicho ni wezi,  amewataka waumini hao kuachia polisi kufanya uchunguzi wa tukio hilo.
Katekista wa kanisa hilo, Joseph Mwiru, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo usiku wa kuamkia juzi na kwamba, watu hao walijisaidia mafungu matatu ya kinyesi huku fungu moja lilikuwa  sehemu karibu anaposimama katekista, eneo la altare na karibu na meza ya kuandalia sadaka.
Pia, alisema walifanya uharibifu mkubwa wa mali za kanisa na kuiba sanamu ya Bikira Maria, vitabu vitatu vya Biblia, visonzo vya sadaka viwili na  kisado  cha kuhifadhia maji ya baraka.
 Vitu vingine vilivyoibwa ni meza, kiti, vibao tisa  ambavyo ni vituo vya Yesu, sanamu ya Yesu, kanzu tatu anazovaa Katekista na misalaba miwili inayotumiwa kanisa hapo.
Alipoulizwa kama uharifu huo unahusishwa na imani ya kidini, kiongozi huyo alikanusha na kusema kuwa ni mapema mno kuhisi kuwa kuna chuki za kidini kati ya waumini wa dini za kiislamu na Kikristo balianachoweza kusema kuwa ni uhalifu wa kawaida.
Alisema kuwa baada ya kupata taarifa za tukio hilo waumini wa kanisa hilo kijijini hapo walikusanyika na kuanza kutafuta mali zao katika maeneo ya jirani na kanisa hilo na kufanikiwa kupata meza moja iliyoharibiwa miguu yake, kabati moja sanamu ya bikira maria na misalaba ikiwa imetupwa porini na biblia zikiwa 
chanzo:mwananchi

0 comments: