MAJAMBAZI WALIOMJERUHI NA KUMPORA MWANACHUO UDSM YAKAMATWA

0


WATUHUMIWA wanne wa ujambazi uliotokea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kusababisha majeruhi wamekamatwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Ally Mlege alisema majambazi hao walikamatwa Julai 8, mwaka huu katika eneo la Ubungo kituo cha daladala ambapo askari waliweka mtego wa kuwakamata.

Kamanda Mlege alisema baada ya kukamatwa kwa watuhumiwa hao walipopekuliwa walikutwa na simu na bunduki aina ya Shot Gun ikiwa na risasi moja, kompyuta mpakato mbili Toshiba, simu ya mkononi Samsung C3230, panga pamoja na nyundo.

Alisema baada ya kuhojiwa , inadaiwa walikiri kuhusika na tukio la unyang'anganyi kwa kutumia silaha la Juni 21, mwaka huu katika Bweni la Yombo One na kumjeruhi mwanafunzi huyo kwa risasi tumboni kisha kupora mali mbalimbali.

"Mbali na tukio hilo pia wamekiri kuhusika na matukio ya uporaji maeneo ya Ubungo Darajani, Chuo Kikuu na maeneo mengine, ni wahalifu wazoefu sasa tunaendelea na upelelezi ili kuwafikisha mahakamani," alisema Kamanda Mlege na kutaja majina ya watuhumiwa hao ambao watafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika.

Alisema watuhumiwa hao walipopekuliwa nyumbani kwao walipatikana na mabegi 16 ya kuhifadhia kompyuta mpakato, flashi diski tatu pamoja na vitu vingine ikiwemo kitambulisho cha mwanafunzi wa chuo kikuu aitwaye Kapalata John.

Katika hatua nyingine, Kamanda Mlege alisema katika tukio jingine, polisi walifanikiwa kukamata bunduki mbili aina ya Shot Gun na bastola tano ambapo mbili kati ya hizo zilihusika katika mauaji katika eneo la Mbezi NHC.

Bunduki hizo zina namba TZ CAR 59215 ikiwa na risasi nane na tatu zikiwa kwenye kasha la sigara; Nyingine ni yenye namba TZ CAR 79516 ikiwa na risasi tatu zikiwa zimetekelezwa jalalani.

Alisema baada ya uchunguzi kufanyika iligundulika watuhumiwa Michael Paschal (35), Donald Joseph (43), Kulwa Adamson (43), Ally Akiri (41) na wenzao watano walirushiana risasi na askari katika eneo la Kunduchi Mtongani.

Baada ya kufuatiliwa, inadaiwa walikamatwa wakiwa na mapanga saba waliyokuwa wameyaficha kichakani pembeni mwa mto Nyakasagwe katika eneo la Boko Dovya

0 comments: